Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mkongwe wa bongo fleva nchini Madee Ali amefunguka na kuweka wazi kwamba adhabu kubwa aliyowahi kupatiwa na katika maisha yake ni pamoja na kupigwa kofi na baba yake lililompelekea kupoteza fahamu kipindi akiwa mwanafunzi wa shule ya mnazi mmoja.

amesema kwamba kipindi akiwa mwanafunzi alikuwa akitumia muda mwingi kuzurura kwenye daladala hali iliyokuwa ikimfanya kuwa mtoro kwa hata zaidi ya miezi shuleni.
Madee amesema kwamba kibao alichopigwa na baba yake alikipata akiwa ametoroka shule akiwa zake njiani mitaa ya Kariakoo akiwa tayari ameshabadilisha nguo za shule.
Mkongwe huyo anasema alipokutana na Mzee Ali mitaa ya Kariakoo alinaswa kofi ambalo lilimpa nyota nyota na baada ya hapo alikuja kushtuka akiwa mbele ya wanafunzi wenzake wakimcheka hukui wengine wakimshangaa kwa kutoonekana darasani zaidi ya mwezi mmoja wakati baba yake alikuwa akimpeleka kila siku shuleni.
Hata hivyo Madee amesema kuwa baada ya adhabu hiyo baba yake hakurudia kumpiga tena.
 

Post a Comment

 
Top