Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
SIKU chache baada ya staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ kufungiwa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutofanya sanaa miezi sita kutokana na wimbo wake wa Kibamia kukosa maadili, msanii mwenzake, Pamela Daffa ‘Pam D’ amehuzunishwa zaidi na mke wa staa huyo aitwaye Nancy kwani ni mjamzito.

Pam D ambaye yupo chimbo akiandaa ngoma yake yenye mahadhi ya Singeli alisema, taarifa za kufungiwa kwa Roma zilimpa mshituko mkubwa na kujikuta akivaa uhalisia wa mshituko huo na alioupata Nancy ambaye yupo kwenye harakati za mwisho za kujifungua.

“Hii ishu imeniumiza, sababu Roma maisha yake yanate-gemea sanaa ya muziki na kipindi hiki alikuwa bize akisaka pesa kwenye shoo mbali-mbali ili aweze kumlea vyema mtoto wake atakaye-zaliwa. Dah! Namu-ombea sana Nancy ajifungue salama na hili litapita tu!”alisema.

Post a Comment

 
Top