Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

BAADA YA video yake kusambaa akiwa anakata mauno kihasarahasara stejini na watu kuhoji inakuwaje mke wa mtu kufanya hivyo, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameibuka na kufunguka kuwa haoni shida kwani hata mumewe anajua anakichofanya.
 Shilole au Shishi Baby alisema kuwa, anawashangaa wanaozungumza kuhusu kukata mauno kihasara jukwaani, wakati wanatakiwa kufahamu kwamba ile ni kazi yake hivyo hata mumewe analiheshimu hilo kwamba yupo kazini.

“Mume wangu Uchebe (Ashraf) anajua nikiwa kazini, chochote naweza kufanya jukwaani, haoni shida maana ananipenda na kazi yangu hivyo wanaosema ninawasihi waache kwani pale nilikuwa kazini kwa hiyo lazima niwapagawishe mashabiki wangu,” alisema Shilole.

Post a Comment

 
Top