FRANK Mshumbusi almaarufu Fraga ambaye ndiye prodyuza wa Wimbo wa Happy Birtyhday wa msanii kutoka Wasafi , Harmonize amejiweka kwa msanii Snura ambapo hivi karibuni wawili hao walionekana wakiwa wamegandana
Fraga ambaye kwa sasa ameingia rasmi kwenye gemu la Bongo Fleva huku wimbo wake wa Kimwali ukiwa gumzo kwenye redio na runinga mbalimbali Bongo, alisema ukaribu wake na Snura ni kuhusu kazi na kwamba wanatarajia kuja na ‘projekti’ ya pamoja.
“Nimemfahamu Snura tangu kitambo na huwa navutiwa na kazi zake ndiyo maana nilipokutananaye Studio za Global TV,nilimganda kwa lengo la kuyajenga kwasababu nataka nimshirikishe kwenye ‘project’yangu,” alisema Fraga ambaye anasimamiwa kimuziki na Nambiza Enterprises.







Post a Comment