Wakurugenzi wawili wa halmashauri za Kigoma Ujiji, pamoja na Pangani wamesimamishwa kazi kuanzia leo na Rais Magufuli baada ya manispaa ya zao kukutwa na hati chafu baada ya kufanyiwa ukaguzi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo ya utenguzi leo wakati akipokea ripoti kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali, Profesa Musa Assad ambapo ripoti hiyo imeonyesha manispaa hizo kuwa na hati chafu.
Amesema kwamba ameamua kuchukua hatua hizo kwa sababu wameaibisha serikali na anaamini kupitia wakurugenzi hao litakuwa fundisho kwa wengine.
Mh. Rais amesema kuwa siyo vizuri sana kufanya utenguzi lakini lazima hatua zichukuliwe kwani hata wenyeviti wa kamati za bunge wamemshauri kuchukua hatua kwani "Tusipochukua hatua hatutafika".







Post a Comment