Wasanii Nikki Mbishi na Moni
wa Centrozone wametupiana maneno baada ya hivi karibuni Nikki kusema kuwa kundi
jipya la Moni linalofahamika kama MOCO ni lakupita tu wala haliwezi kufika
mbali.
Moni amesema kwamba anamshangaa sana Nikki amekuwa ni mtu
wa kulalamika na lawama huku akiongeza kuwa siku hizi hata kazi za Nikki
hazioni zaidi anasikika akiwa analalamika tu.
Moni amesema
yeye na kundi lake hawafanyi Rap ya kilingeni bali anafanya Rap ya biashara
hivyo hayo maneno ya Nikki wala hayamsumbui kwasababu tayari wamefanya kazi
nyingi na wanashukuru Watanzania wamewapokea.
Kwa upande
mwingine Moni ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Nichum amesema
kinachomsumbua Nikki ni uzoefu wake wa kuvunjikiwa na kundi kutokana na uzembe
wake huku akimshauri kuwa afanye kazi kwa bidii kwa kuwa anamizizi mizuri na
nimuandishi mzuri hivyo asimamie sanaa yake kwanza.







Post a Comment