Msanii
wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa
mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo
maana anakurupuka katika baadhi ya mambo.
Wastara amesema hayo kuwa Mange Kimambi alizusha juu
ya Cannula aliyowekwa mkononi na kusema alijiwekea mwenyewe, Wastara amesema
kuwa mbali na kuzusha huko lakini dada huyo alikwenda mbali mpaka kuwauliza
madaktari wa hospitali aliyokuwepo kama anatibiwa hapo.
"Mange
Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja
wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa
kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye
Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi
nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe"alisema Wastara
Mbali na hilo
Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa
kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa
vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha.







Post a Comment