Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rapa wa kike anayefanya vizuri na kibao chake chake cha  'Dow', Rosa Ree amesema hajawahi kutoka kimapenzi na msanii mwenzake Young Dee hata mara moja na kudai kwa sasa hana hisia za kufanya hivyo kwa kuwa anahasira ya kutafuta pesa nasio mapenzi
Rosa Ree ametoa kauli hiyo baada ya kuonesha picha mitandaoni zikiwaonesha wawili hao wakiwa pamoja muda mrefu katika sehemu mbalimbali nje ya Dar es Salaam na kupelekea baadhi ya watu kudai wawili hao wanatoka kimapenzi kwa sasa na wameshalala pamoja.

"Sijawahi kufanya kitu na Young Dee, nilikuwepo naye kwenye 'show' tukapiga 'tour' lakini hatujawahi kutoka kimapenzi", amesema Rosa Ree

Pamoja na hayo, Rosa Ree ameendelea kwa kusema "mimi hayo mambo kwanza sinaga, siwezi kufikilia hayo mambo sasa hivi, nawaza sana pesa kwa hiyo 'i don't have time for that', sijisiki kabisa yaani kama hizo hisia za kufanya mapenzi sina kabisa. Siku nikifanikiwa kupata hela sana na nikifika ninapotaka ndio labda nitalainika kidogo lakini kipindi bado sana".

Kwa upande mwingine, rapa huyo amefanikiwa kutambulisha wimbo wake mpya  iliyopewa jina la 'Marathon' ambayo amemshirikisha msanii Bill Nass.

Post a Comment

 
Top