Spika
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amefanya
mabadiliko ya kamati mbalimbali za kudumu za bunge kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
Taarifa ya bunge iliyotolewa leo imesema kuwa ibara hiyo ya 96,
imelipa uhalali Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania kuunda kamati za Bunge
za namna mbalimbali kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa
madaraka yake.
Aidha ibara
hiyo imeweka wazi kwamba kanuni za kudumu za Bunge zitafafanua muundo wa shughuli
za kamati za Bunge.
Kwa msingi huo
kanuni ya 118 ya kanuni ya kudumu za Bunge, toleo la Januari 2016 imeweka
kamati za kudumu za Bunge zenye muundo wa majukumu mbalimbali kama
yanavyofafanuliwa kwenye nyongeza ya nne.
Uteuzi wa
waunge kwenye kamati mbalimbali umewekwa utaratibu katika kamati ya 116 . Aidha
kanuni ya 116(7) inaweka utaratibu kwamba ,ujumbe kwenye kamati za kudumu za
Bunge utadumu mpaka mwisho wa mkutano wa kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza
ya maisha ya Bunge.
Ikumbukwe
kwamba mnamo tarehe 21 Januari 2016 kupitia waraka wa Spika wa Bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai namba 02/2016 alifanya
uteuzi wa ujumbe katika kamati mbalimbali za Bunge.
Ambapo kamati
hizo zimetekeleza majukumu yake mpaka tarehe 9 Februari , 2018 ambapo ni mwisho
wa mkutano wa kumi wa Bunge ambao unakamilisha nusu ya uhai wa Bunge la kumi na
moja. Hivyo kwa mujibu wa kanuni ya 116(7), kipindi hicho ndio ukomo wa ujumbe
katika kamati walizokua wakizifanyia kazi wabunge.
Hivyo kwa
mamlaka aliyopewa Spika na kanuni ya 116(3) na kwa kuzingatia vigezo
vilivyoainishwa katika kanuni ya 116(5) amefanya uteuzi mpya wa wajumbe katika
kamati za kudumu za Bunge na wajumbe wa kila kamati ya kudumu wanawajibika
kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kanuni ya 116(10) kuwa
viongozi wao.







Post a Comment