Mwanasheria
Jebra Kambole na Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP),
Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa ameshindwa kuonana wala
kuongea na mteja wake huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi.
Wakili huyo amesema kuwa amejaribu kufika ofisi ya Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kujua hali ya mteja wake pamoja na
kuweza kuongea naye lakini ameshindwa.
"Mpaka
sasa sijafanikiwa kuzungumza wala kumuona kwa sababu mara ya mwisho wakati
tunafanya mazunguzo na DCI ambaye ana mamlaka juu ya hilo kwa sababu Abdul
Nondo alikuwa anashikiliwa ofisini kwake mpaka dakika ya mwisho, tulipokwenda
ofisini kujaribu kumuona akasema sisi huyu mtu tunamshikilia kama kama
mlalamikaji lakini siyo kama mtuhumiwa kwa hiyo nyinyi kama Mawakili hamtakiwi
kumhoji ila tukiona kwamba huyu mtu ni mtuhumiwa basi tutawaita muweze kuongea
naye na kusikiliza maelezo yake, sisi tulimweleza tunahitaji kumuona ili tuweze
kujua afya yake ili tuweze kurejesha mrejesho kwa familia na Watanzia wengine
kwa ujumla ambao wanahofia juu ya usalama wake akasema yupo salama" alisema Kombole
Aidha Wakili
huyo aliendelea kudai kuwa mpaka sasa Abdul Nondo anashikiliwa kinyume na
sheria kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai haitoi ruhuusa kwa jeshi la polisi
kumshikilia mlalamikaji.
"Anayeshikiliwa
ni mtuhumiwa lakini mpaka siku ya leo hajaachiwa kama ni mtuhumiwa kweli kwa
sababu mtu ambaye anakwenda kutoa taarifa polisi anaachiwa arudi nyumbani
huwezi kushikiliwa huko polisi na kwa kuwa wao wanasema wanamshikilia ana haki
ya kupata uwakilishi kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya mwenendo wa makosa
ya jinai sura namba 20 ya sheria za Tanzania, kifungu cha tano kinasema kwa
muda gani mtu atakuwa chini ya dola au polisi, mtu ambaye amewekwa chini tu
akiwa hana uhuru wa kwenda anakotaka huyo ina maana yupo chini ya ulinzi kwa
hiyo kama upo chini ya ulinzi una haki ya kupata wakili kuweza kuongea naye na
kujua nini kinaendelea na hatma yake na kupata fursa ya kuongea na ndugu zake
na familia lakini fursa hiyo kwa Nondo haijapatikana kwani saizidi ni zaidi ya
masaa 10 yamepita akiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi" alisema
Kombole
Mbali na hilo
Wakili huyo amesema kuwa mpaka sasa wao hawajui Abdul Nondo ameshikiliwa kwa
sababu zipi na kusema kuwa kijana huyo ameshikiliwa kinyume na sheria, kinyume
cha Katiba, kinyume cha haki za binadam na kinyume na utaratibu wetu kama taifa
kiujumla.







Post a Comment