Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amemsimamisha kazi Mhifadhi Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Kanda – Pori la Akiba Rukwa lililopo wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, Emmanuel Barabara ili kupisha uchunguzi uendelee dhidi yake
Dkt. Kigwangalla amechukua uamuzi huo kufuatia taarifa za raia wema kuwa Bwana Barabara amekuwa akishirikiana na majangili katika kuhujumu rasilimali za misitu nchini.

Aidha, Waziri Kigwangalla ameagiza iundwe Kamati ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo, na endapo mtuhumiwa huyo atakutwa na hatia, hatua kali za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ili iwe fundisho kwa wengine.

Post a Comment

 
Top