MACHI 1, mwaka huu ni mwezi usiosahaulika katika maisha ya Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ katika Muziki wa Hip Hop Bongo mara baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kumfungia kutojihusisha na shughuli zozote za muziki kwa muda wa miezi sita baada ya kukaidi kufanya marekebisho wimbo wake wa Kibamia.
Hata hivyo, Machi 29, mwaka huu, Waziri Harisson Mwakyembe alitangaza kumfutia adhabu hiyo baada ya kukamilisha taratibu za kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kukubali wimbo wake usiendelee kupigwa katika vituo vya redio na TV.
Ukiachilia hayo, tukio jingine ambalo Roma hatalisahau ni siku moja baada ya kufunguliwa kufanya muziki yaani Machi 28, mkewe, Nancy alijifungua mtoto wa kike na kuongeza furaha katika familia mbapo hadi sasa ana watoto wawili akiwemo wa kwanza ambaye ni wa kiume anayeitwa Ivan.







Post a Comment