Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo baada ya kufiwa ya mama yake mzazi usiku wa kuamkia jana.

Zitto amesema kuwa anajua uchungu wa kupotelewa na mama huku akieleza kuwa hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.
Pole sana kwa Msiba huu mkubwa ndugu Mrisho Gambo. Najua uchungu wa kupotelewa na mama. Hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi. Mola akupe subira wewe na ndugu zako. Inna lilah waina ilaih raajiun ameandika Zitto kwenye mitandao yake ya kijamii.

Post a Comment

 
Top