Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Monalisa Achaguliwa Katika Tuzo Nchini GhanaMuigizaji mkongwe katika tasnia ya Bongo movie nchini Monalisa amefanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za African Prestigious Awards nchini Ghana zitakazofanyika April 14,2018 na kukabidhiwa bendera ya Taifa na ticket ya ndege kutoka Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya safari yake.


Monalisa alisindikizwa na mama yake mzazi katika makabidhiano hayo katika ofisi za BASATA na makabidhiano hayo yalihudhuria na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu mtendaji wa BASATA Godfrey Mwingereza.



Monalisa ametoa shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote waliompigia kura na kusema kuwa hata asiporudi na ushindi lakini ana amini kuwa haiwezi kukosekana tuzo ya Ray Kigosi, Mzee Majuto au Moiz Hussein na kuahidi kutuwakilisha Watanzania vizuri kwa kuipeperusha bendera ya Taifa.

Post a Comment

 
Top