Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Raia Mwema, Paschal Mayallah pamoja na Wahariri wa gazeti hilo wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyochapishwa Jumatatu Aprili 9, 2018 .

RM.jpg
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 12, 2018 na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika mnamo Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari kilichosomeka ‘BUNGE LINAJIPENDEKEZA?’ haidhalilishi bunge.
Mwandishi huyo na Wahariri wa gazeti hilo wanatarijiwa kuhojiwa mapema iwezekanavyo ili kuweza kubaini kama maudhui ya makala hayo.

Post a Comment

 
Top