Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwigizji na msanii wa bongo movie Irene Uwoya ameipongeza kampuni ya Itel kwa kutimiza miaka 10 katika huduma zake huku ikiwa imehudumia zaidi ya nchi 45 na ikuza simu zaidi ya milioni 100.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Itel Mobile Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo amesema kuwa wanayo furaha kutimiza miaka10 kama anavyonekana kwenye picha.

Kampuni ya Simu ya Itel Mobile imetimiza madhamisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku ikiendelea kufanya vizuri katika soko la mauzo ya Simu na kuwa kinara kwa ubora wa bidhaa zake barani Afrika na nje ya Afrika.

Miaka 10 iliyopita Itel Mobile ilizindua mpango wa kumwezesha kila mmoja kuwa na simu bora kwa ajili ya mawasiliano ya uhakika,katika kipindi hicho chote tumepitia katika kipindi kigumu katika Nyanja za kiuchumi na kisiasa lakini tumeweza kufanikiwa kutimiza mlongo mmoja kwa uthabiti mkubwa.

Ndani ya miaka 10 Itel Mobile imekuwa na mabadiliko makubwa chanya ya bidhaa kutokana na kufuatwa matakwa ya wateja wake hivyo imepelekea kupendwa na kuleta mvuto kutokana na kuboreshwa kwa bidhaa hizo kwa ubunifu mkubwa.

”Tumeweza kuongeza idadi ya wateja mara mbili zaidi barani Afrika na pia shukrani zetu za dhati ziende kwa wateja wetu pamoja na mashabiki wote wa Itel na mpaka sasa tumeuza jumla ya simu milioni 100’alisema Makamu Rais

Aidha nguvu kubwa yetu inatokana na bidhaa zetu zilivyo bora pamoja na timu ya wafanyakazi wetu ambao kila mmoja amekuwa akijituma kutokana na nafasi yake na pia ubora na mvuto wa bidhaa unatokana na mapendekezo ya watumiaji wetu na huduma za matengenezo baada ya mauzo na warantii ya miezi 12 kwa bidhaa zetu zote.

Hata hivyo tumekuwa na ushirikiano na mastaa wa nchi za Afrikia kama mabalozi wa kampuni yetu na wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni ya Itel ambapo imekuwa kampuni 3 bora barani Afrika.

Na kwa kuonesha upendo wetu Afrika tumekuwa tukifanya matendo ya ukarimu kwa jamii na kujitolea kutembelea baadhi ya shule na vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.

Post a Comment

 
Top