Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PIC 1b
Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge  Mhe. Almasi Athuman  Maige (Mb), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kumhoji Mhe. Saed Kubenea (Mb) kwa kosa  la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)  ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.  Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati hiyo leo ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuomba  mahojiano yake yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.

pic 2a
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea (Mb) akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge  kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)  ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea amefika mbele ya Kamati hiyo leo kwa mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano hayo yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.
Kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji  Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.
 
Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa  Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati  hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho   ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)   ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. 
 
Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika  leo baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe. 
 
Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa  baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.
 
“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.

Post a Comment

 
Top