MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI (R) SEMISTOCLES KAIJAGE AMESEMA WAZIRI WA TAMISEMI AMEITAARIFU TUME KUWEPO NAFASI WAZI KATIKA KATA TANO KATIKA HALMASHAURTI MBALIMBALI NCHINI.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiitaarifu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia Ndugu Lazaro Samwel Nyalandu kuvuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.
Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo Ndugu Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
Wakati huo huo Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
| NA. | MKOA | HALMASHAURI | JIMBO |
| 1. | Singida | Halmashauri ya Wilaya ya Singida | Singida Kaskazini |
| 2. | Arusha | Halmashauri ya Wilaya ya Longido | Longido |
Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
| NA. | MKOA | NA. | HALMASHAURI | NA. | KATA |
| 1. | Kagera | 1. | Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. | 1 | Keza |
| 2. | Arusha | 2 | Halmashauri ya Jiji la Arusha | 2 | Kimandolu |
| 3. | Pwani | 3. | Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. | 3 | Kurui |
| 4. | Tabora | 4. | Halmashauri ya Wilaya ya Tabora | 4 | Bukumbi |
| 5. | Tanga | 5. | Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. | 5 | Kwagunda |
Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
16 NOVEMBA, 2017






Post a Comment