Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wadau wa maji uliandaliwa na benki ya Dunia nchini uliokwenda kwa jina la 'TANZANIA WASH POVERTY DIAGNOSTIC' uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Malawi na Burundi, Bella Bird akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji kufungua mkutano huo muhimu kwa ajili ya maji Tanzania.
Mwasilishaji wa mada juu ya kupinga umaskini na uhaba wa maji Mchumi wa Benki ya Dunia, George Joseph akizungumza na wadau wa maji waliofika katika mkutano huo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini(TUDARCO), Prof. Uswege Minga akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa utunzaji wa maji na na mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.
Baadhi ya Wadau wa Maji wakifatilia kwa ukaribu Mkutano wa Benki ya Dunia wa masuala ya maji uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji.
WAZIRI
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ni muhimu
kuwekwa mikakati ya kukabiliana na uharibifu unaoendelea katika vyanzo
mbalimbali vya maji na misitu nchini.
Mhandisi
Kamwele amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya
Wiki ya Maji Duniani na kwa Tanzania lengo lake ni kuangalia uwezekano
wa kuwapatia maji safi na salama kwa watanzania wote.
Aidha
ameeleza mkakati wa kuvuna maji ya mvua ili kupata maji shuleni kupitia
matanki na visima vya kujenga ambapo anaamini itasaidia kuondoa
changamoto ya uhaba wa maji shuleni.
Pia
ameeleza mafanikio katika suala la maji na majengo katika shule za
Kirumba na Isenyi jijini Mwanza pia katika ujenzi wa vyoo na vyumba kwa
wanafunzi wa kike.
Ameshukuru
Benki ya dunia, Serikali ya Korea na Mpango wa maendeleo Ufaransa kwa
ushirikiano wao katika suala la maji na utunzaji wa mazingira na vyanzo
vya maji ni lazima.
Amesisitiza
Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuleta mapinduzi katika
kutokomeza umaskini ikiwemo katika kutatua suala la upatikanaji wa maji.
Pia amehimiza ushirikiano baina ya wanajamii katika suala la ukataji miti na uharibifu wa misitu.
Naye
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Profesa Uswege Minga amesisitiza
utunzaji wa maji kwani matumizi yake ni makubwa zaidi ya kupika na
kunywa na amesisitiza utunzaji wa maji na vyanzo vyake sambamba na
matumizi sahihi ya maji.






Post a Comment