Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hiki Hapa Kikosi cha Taifa Stars Kitakachokabiliana na Algeria, DR Congo

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Soka Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga, leo Machi 8, ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki mwezi huu.

Katika orodha hiyo aliyoitaja asubuhi hii kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF Karume Ilala, Mayanga amewajumuisha kikosini nyota wanne wa kimataifa akiwemo nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, Mlinzi wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda na Faridi Mussa anayechezea Club Deportivo Tenerife ya Hispania.

Katika majina hayo 23 Simba imeongoza kwa kuchangia wachezaji wengi zaidi ambao ni 6 huku Yanga ikitoa wachezaji 5 huku nahodha wa Singida United Mudathir Yahya naye akijumuishwa kikosini

Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ikianzia ugenini nchini Algeria Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha DR Congo Machi 27 Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

 
Top