Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii mkongwe wa filamu nchini Tanzania, Blandina Chagula maarufu kama Johari amedai haangalii sana mahusiano na mwanaume mwenye pesa nyingi wala muonekano mzuri aliokuwa nao kwasababu vitu hivyo vinatafutwa.
Johari amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu miongoni mwa maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mashabiki zake waliokuwa wanataka kufahamu ni mwanaume wa aina gani Johari anamvutia kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi.

"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambaye anajituma katika ufanyaji wa kazi, awe na hofu ya Mungu, atakayeweza kunipenda mimi kutoka moyoni pamoja na kuthamini kazi yangu mimi ya sanaa ninayoifanya. Kwasababu mtu mwingine anaweza akaiona haina maana wakati mimi nisingekuwa hapa bila ya hii sanaa", amesema Johari

Pamoja na hayo, Johari ameendelea kwa kusema "siwezi kumtaka mwanaume kutokana na muonekano wake wa sura au rangi pia siwezi kumpenda kutokana na pesa maana hivyo vitu vinatafutwa".

Post a Comment

 
Top