Rais Dkt. John Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango ashirikiane na jopo la Majaji ili kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu Mahakamani kusudi kuweza kuokoa kiasi cha fedha zilizopo katika kesi hizo ziweze kutekelezea mambo mengine.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Machi 27, 2018) wakati alipokuwa anapokea ripoti kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Profesa Musa Assad hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
"Nimuombe Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwenye zile kesi ambazo zimekaa 'pending' za kodi, mshirikiane na Jaji Mkuu pamoja na Jaji Kiongozi ili kusudi mzimalize. Nina uhakika mtazimaliza hata mkitengeneza 'task force' ya majaji mkalizimaliza hizi kesi kwasababu ni kweli zimekaa kwa muda mrefu", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "ninafahamu mna upungufu wa Majaji, na mimi naendelea kuchambua chambua ili kusudi tupate hiyo ila tutakujadiliana ili kusudi nije kuteua baadhi ya Majaji waje kukuongezea nguvu lakini angalau unisaidie kwenye hili kwasababu kuna Trilioni 4.4. Kwa hiyo hata nikiteua Majaji ninaweza kukosa pesa za kuwalipa na kuwanunulia magari basi hebu nisaidie kwenye hili angalau. Judgement ya haya ambapo tunaweza kuokoa Trilioni 4.4, zitusaidie kwenye kuendesha nchi kwasababu muda mwingine haya mambo yanategemeana. Usipokuja fedha kule basi ujue mambo mengi huwezi kuyamaliza".
Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amesema muda mwingine anashindwa kufanya jambo lolote kutoka na kutokuwa na fedha ambayo itakayoweza kuiwezesha serikali kufanya hivyo huku akitolea mfano, suala la kutoa ajira polisi, kuongeza posho za wabunge na mambo mengine.






Post a Comment