Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limefungua kuchunguza ili kubaini kama ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo alitekwa au alitoa taarifa za uongo.
Nondo, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK” (niko hatarini) ambapo amepatikana akiwa ametupwa barabarani Mafinga mkoani Iringa na baada ya kuzinduka, imeelezwa alijikokota na kuelekea Kituo cha Polisi Mafinga kuripoti.












Post a Comment